Header Ads

Malawi yawa nchi ya kwanza kuwapa watoto chanjo ya Malaria


Shirika la Afya Duniani(WHO) limesema Malawi imekuwa nchi ya kwanza kuwapa Watoto kinga dhidi ya Malaria, ugonjwa unaoua takribani Watu 435,000 kila mwaka Afrika huku wengi wakiwa ni Watoto chini ya miaka 5.

Shirika limeeleza kuwa japokuwa chanjo hiyo inalinda kwa uwiano wa 1:3 kwa Watoto waliopewa chanjo, ila wale wote waliochanjwa wanatarajiwa kutougua ugonjwa huo kiasi cha kuwafanya kuwa mahututi.

Alister Craig, Mkuu wa Kitengo cha Sayansi katika Shule ya Udaktari ya Liverpool akizungumzia chanjo hiyo amesema "Sio chanjo iliyokamilika lakini bado ina uwezo wa kuokoa maisha ya maelfu ya Watu".

Chanjo hiyo ijulikanayo kama Mosquirix, ilitengenezwa na GlaxoSmithKline na mwaka 2015 Mamlaka ya Dawa Ulaya iliidhinisha matumizi yake huku majaribio ya awali yakionesha chanjo hiyo ilikuwa inafanya kazi kwa 30% kwa watoto waliopewa dozi.

Pedro Alonso, Mkurugenzi wa Mpango wa Kupambana na Malaria kutoka WHO amesema wiki chache zijazo Kenya na Ghana zitaanza kutumia chanjo hiyo, lengo ikiwa ni kufikia watoto 360,000 kila mwaka kwenye nchi hizo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.