Header Ads

Mama amuacha mtoto wa mwaka mmoja na miezi 5 kwenda klabu kwa madai ya kutafuta fedha za kumtunza
MAKETE: Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 5 (jina linahifadhiwa) ameachwa na mama yake ndani usiku, na mama huyo kwenda kujiuza Kwenye klabu za usiku maarufu kama (Night Club) kwa madai ya kutafuta fedha za kumtunza mtoto huyo.

Tukio hilo limefanywa na mama huyo aliyejulikana kwa jina la Diana Joel Kyando (22) usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Dombwela katika mji mdogo wa Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe ambapo majirani ndio waliomtoa mtoto huyo ndani baada ya kumsikia akilia kwa muda mrefu usiku


Akizungumza kwenye ofisi za Afisa Mtendaji kata ya Iwawa wakati akihojiwa na Afisa mtendaji wa Kata hiyo Devota Paul, mama huyo amesema ugumu wa maisha na kukosa fedha za matunzo kutoka kwa baba wa mtoto ndicho kimemfanya kufikia uamuzi huo wa kwenda kujiuza ili apate fedhaJirani Bibi Alatwegha Sanga aliyemsikia mtoto huyo akilia kwa muda mrefu ameelezea namna tukio hilo lilivyotokea na alivyoshirikiana na majirani kumnusuru mtoto huyo


Afisa mtendaji wa Kata ya Iwawa Devota Paul amesikitishwa na kitendo hicho na kuitaka jamii kufichua vitendo kama hivyo ili hatua zichukuliwe kwa kuwa vitendo kama hivyo vimekuwa vikitokea lakini vinafumbiwa macho na wanajamii wenyewe


Kwa upande wa jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia wametoa kauli kuhusiana na tukio hilo


Mpaka tunaondoka eneo la tukio mama wa mtoto huyo alikuwa akishikiliwa kwa mahojiano na mtoto amekabidhiwa kwa Afisa maendeleo ya jamii kata ya Iwawa Ana Mwajeka aendelee kumtunza kwa muda wakatia hatua zingine za kulishughulikia suala hilo zikiendelea


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.