Header Ads

Man United Imewaombea Mashabiki Wake Ulinzi Maalum Nou Camp

Man United Imewaombea Mashabiki Wake Ulinzi Maalum Nou Camp
Club ya Man United ambayo April 16 2019 itacheza mchezo wake wa marudiano wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Nou Camp, imeomba ulinzi wa ziada wapewe mashabiki wake ambao watasafiri na timu kutoka Manchester hadi Barcelona kuisapoti timu yao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia taarifa za mwaka uliyopita za kudaiwa mashabiki wa Chelsea hawakupata ulinzi wa kutosha, hivyo Man United inayotarajia kuwa na mashabiki 4500 watakaokwenda kuisapoti timu yao, wameichukua tahadhari hiyo ili isifike sehemu wakadhurika.

Chelsea walilalamika kuwa walinzi wa FC Barcelona waliwafanyia kitendo cha ukatili mashabiki wake mwaka uliopita, ambapo shabiki wa Chelsea alionekana akipigwa na mlinzi wa uwanja wa Barcelona, Man United wanahitaji ushindi katika mchezo huo ili kutinga nusu fainali kutokana na mchezo wao wa kwanza Old Trafford walipoteza kwa goli 1-0. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.