Header Ads

Marekani yapendekeza ushuru mpya kwa bidhaa za EU


Marekani imetishia leo kuziwekea ushuru wa hadi dola bilioni 11.2, bidhaa mbalimbali za mataifa ya Umoja wa Ulaya, kama kama jibu kwa ruzuku inayotolewa kwa kampuni inayotengeneza ndege ya Airbus.

Kwa zaidi ya miaka 14, Marekani na Umoja wa Ulaya zimekuwa zikishutumiana kwa kutoa ruzuku kwa Boeing na Airbus, katika mzozo wa kulipizana kisasi.

Katika taarifa jana, ofisi ya mwakisilishi wa kibiashara wa Marekani imesema shirika la biashara duniani limegundua mara kadhaa kwamba ruzuku zinazotolewa na Umoja huo kwa Airbus zimesababisha athari kadhaa nchini Marekani.

Mwakilishi huyo wa biashara wa Marekani Robert Lighthizer amesema kesi hii imekuwa katika upatanishi kwa miaka 14, na muda umefika sasa wa kuchukua hatua.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.