Header Ads

Mbenge CHADEMA na CCM waungana kumsaidia mtoto huyuWabunge wa mkoa wa Manyara, Anna Gidarya (CHADEMA) Ester Mahawe na Paulina Gekul (CCM) wameungana kwa pamoja kumsaidia mtoto Joseph Shabani kupata matibabu baada ya kupata ugonjwa wa jabu uliepekea mguu wake wa kulia kuvimba.

Mkuu wa wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu amesema amefurahishwa na umoja waliouonyesha viongozi hao wa kisiasa  katika kumchangia kijana huyo ambaye amepata tatizo hilo.

Amesema aliona picha kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambapo aliguswa na jambo hilo ndipo alipoamua kuchangia kisha kufuatilia ili kujua iwapo amefikishwa hospitali. Aidha amesema serikali itagharamia usafiri wa kwenda na kurudi hospitali ya Muhimbili.

Kijana huyo (20) anamtegemea mama yake pekee ambaye hana uwezo wa kifedha na baba yake alishafafariki dunia. Inaelezwa kuwa alihitimu darasa la saba mwaka 2017 shule ya msingi Masware.

Awali  suala la mtoto huyo liliibuliwa na Mbunge Anna Gidarya baada ya kupata taarifa za mtoto huyo kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, George Bilingi baada ya kurekodi Clip fupi ya Video na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii akimshirikisha Mwandishi Charles Masayanyika wa ITV.
Kwa upande Mbunge wa viti maalum, Ester Mahawe akionyesha kugushwa na tatizo la mtoto huyo aliendelea kuhamasisha watu kumchangia pesa mtoto huyo ambapo ilikuwa ikihitajika Tsh. 600,000  kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC au Mhimbili ambapo pesa zilizopatikana mpaka sasa ni zaidi ya Tsh. 1, 000,000.

Aidhha, Mahawe amesema aliwasiliana na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ambaye aliahidi kutoa gari na mafuta kwa ajili ya kumfikisha katika hospitali atakayoenda kupatiwa matibabu.

Naye Mbunge wa jimbo la Babati mjini, Paulina Gekul alichukua hatua ya kuwasiliana na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Ally Mwalimu ambaye alimueleza kuwa wizra itasimamia matibabu ya kijana huyo. Mbunge mwingine aliyetoa mchango wake ni Flatei Massay wa jimbo la Mbulu vijijini.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.