Header Ads

Mlinzi alalamika kuvamiwa na kupigwa nondo


Mkazi wa kijiji cha Osiri kata ya Roche wilayani Rorya Tumaini Steven (40) ambaye ni mlinzi wa Amani  MUJATA amelalamikia kitendo cha kuvamiwa na kupigwa na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakimtuhumu kuwa  ni Mmoja ya watu ambao walihusika kuwataja kuwa wanajihusiasha na matukio ya wizi wa mifugo.

Akisimulia mbele ya mwaandishi wa habari Steven alisema kuwa watu hao walifika Nyumbani kwake wakiwa kundi la watu sita huku wakiwa wamebeba silaha mbalimbali za jadi zikiwemo Nondo na kuanza kumwaamuru kukaa chini ili kujisalimisha mara baada ya tukio la kukaa chini  walianza kumshambulia kwa kipigo.

“Tukio lenyewe  lilitokea majira ya saa 11 jioni Januari 03,2019 wakati nikiwa  Nyumbani kwangu walikuja watu Sita wakiwa wamebeba silaha mbalimbali za jadi huku wakiwa na Nondo na kuanza kunitaka nijisalimishe baada ya hapo wakaanza kunishambulia sehemu mbalimbali za mwili wangu kwa kipigo na kunisababishia ulemavu wa mikono sasa sifanyikazi”alisema,Steven.

Steven  aliongeza kuwa wasamaria walimsaidia baada ya kusikia makelele ya kilio cha kuvamiwa Nyumbani kwake ambapo walimpa masaada  na kumchukua kwenda  polisi ili kupata barua ya PF3 ya kwenda kutibiwa pia kufungua kesi  ambapo alipewa PF3 pamoja na kufungua polisi yenye namba ya UGI/IR/06/2019.

Pia Steven alifafanua kuwa majambazi hao walikuwa wanadai na kumtuhumu kuwa aliwataja kwenye mkutano wa  Mbunge wa Jimbo hilo Lameck Airo wa mwaka 2018 ulioitishwa kwa lengo la kuwataja wezi wa mifugo ambao ulifanyikia kata ya Kitembe kijiji cha Kitembe kwa lengo la kuwataja wanahusika wa matukio ya wizi wa mifugo Rorya.

Mlalamikaji huyo anasema kuwa watuhumiwa wake wanafahamika kwa  majina na kwa majina ni Tomm Odam,Junga Tomm,Bonn Tom,Okongo Ndege,Goro Siengo na Otiambo Omitiyi  na kuwa majina hayo yapo  polisi lakini cha kushangaza hawajakamatwa  wako nje wakitamba na kumtishia masiaha.

Kwa upande wake Peter Kayemba msahauri wa MUJATA Tarime,Rorya  alisema kuwa mwanachama wake huyo,Tumain Steven kulizuka Ugonvi kati yake na  jirani yake ambapo walianza kurushiana maneno hatimaye wakifikia kujeruhiana .

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.