Header Ads

Moto ulioteketeza kanisa kuu mjini Paris, uchunguzi waanza


Wachunguzi wameanza kufanyakazi leo kutambua chanzo cha moto mkubwa ulioharibu kanisa kuu mjini Paris la Notre Dame, wakati maafisa wa kanisa walikuwa wakichunguza uharibifu uliotokea kutokana na maafa hayo ambayo yameishitua Ufaransa na dunia kwa jumla.

Michango na mapendekezo yameanza kutolewa leo , wakati watu wakishuhudia uharibifu uliotokea katika moto usiku wa jana Jumatatu ambao ulichukua muda wa masaa 15 kuzimwa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alieleza kwamba atalijenga kanisa hilo la Notre Dame kwasababu ndio Wafaransa wanachotarajia.

Wito wa michango kutoka kwa umma umeanzishwa na wakfu wa turathi za Ufaransa kusaidia kulijenga upya kanisa hilo ambalo ni ishara ya historia ya Ufaransa na utamaduni.

 Msemaji wa idara ya zima moto mjini Paris Gabriel Plus amewaambia waandishi habari kwamba uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha moto huo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.