Header Ads

Moto uliozuka kanisani Ufaransa wadhibitiwa


Kikosi cha wazima moto zaidi ya 400 jijini Paris wamefaulu kuudhibiti moto ulivamia majengo ya kanisa kongwe la Notre-Dame, mfumo mzima wa jengo umeokolewa lakini paa lote zimeharibiwa na moto.

Mkuki na paa zima la Kanisa la Notre-Dame, ambalo ni mfano wa mji mkuu wa Ufaransa, ulianguka jioni ya jana kutokana na moto. Hata hivyo moto huo ulidhibitiwa usiku baada ya masaa kadhaa.

Rais wa Ufaransa Emmauel Macron aliahirisha hotuba yake kwa taifa na kuelekea kwenye eneo la tukio ambapo ameahidi kuwa kanisa hilo litajengwa huku akipongeza kuona maeneo muhimu yameokolewa.

Uchunguzi kuhusu kubaini chanzo cha moto huo umeamzishwa na mahakama jijini Paris. Wafanyakazi waliokuwa katika ujenzi uliokuwa ukiendelea katika kanisa hilo tayari wamehojiwa na Polisi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.