Header Ads

Mtu mmoja auawa na Tembo kisha aliwa na Simba


Mtu mmoja aliyeshukiwa kuwa jangili wa wanyama aina ya faru amekanyagwa na Tembo na kuliwa na Simba katika hifadhi ya taifa ya Kruger, nchini Afrika Kusini.

Familia ilipewa taarifa kuwa mtu huyo aliuawa na tembo siku ya Jumanne, Ulipofanyika msako hatimaye fuvu la kichwa cha mtu huyo kilipatikana na suruali siku ya Alhamisi,  Mkurugenzi wa hiadhi hiyo ametoa salamu za rambirambi kwa familia.

''Kuingia kwenye mbuga ya Kruger kinyume cha sheria na kwa miguu si jambo jema,'' alisema Murugenzi huyo. ''ni mbuga yenye hatari nyingi na tukio hili linadhihirisha hayo.''

Hifadhi ya Kruger imekua ikikabiliwa na changamoto ya uwindaji haramu kutokana na uhitaji mkubwa wa pembe za faru kwenye nchi za bara la Asia.

Siku ya Jumamosi, mamlaka za kiwanja cha ndege Hong Kong zilikamata mzigo mkubwa wa pembe za faru, mkubwa zaidi kwa kuwahi kukamatwa katika kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya pauni milioni 1.6.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.