Header Ads

Mwili wa Jessie wa THT Kuzikwa kwao Leo Morogoro

MWILI wa aliyekuwa mwanamuziki wa THT,  Jesca Edward Mahohi ‘Jessie’,  ambaye alifariki Aprili 6 mwaka huu  wakati akijifungua katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, leo umeagwa na mastaa na watu mbalimbali.

Mwili huo umeagwa katika Hospitali ya Mwanayamala na umesafirishwa kuelekea nyumbani kwao Mvomero, Morogoro,  kwa mazishi ambayo yatafanyika kesho.


Jolie ambaye ni mdogo wa marehemu Jessie na akiwa pia ni mwanamuziki wa THT, alizungumza machache kuhusu msiba huo:

“Namshukuru Mungu kwa sababu ni mipango yake kwani sisi binadamu hatujui nini kitatokea,  hiyo ni siri kubwa.  Ila nashindwa kuamini kwa hili. hata hivyo nawashukuru wana THT kwa ushirikiano wao na pia wote ambao wameungana nasi katika kipindi hiki kigumu. Sitaweza kuwataja wote mmoja-mmoja kwa kuwa ni wengi,”alisema.

Picha za chini zinaonyesha hali ya majonzi ya shughuli nzima ya kuuaga mwili huo ilivyokuwa kabla ya kusafirishwa kwenda Mvomero. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.