Header Ads

Papa francis awaonya watu wenye tabia hizi


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameonya dhidi ya mtu kuwahukumu binadamu wengine na kuwa na kiburi, ikiwamo viongozi wa kanisa Katoliki.

 Papa ameyasema hayo katika hotuba yake ya Jumapili ya Matawi wakati wa Misa katika uwanja wa Mtakatifu Peter, uliokuwa umejaa maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali, watalii na wakaazi wa mji wa Roma.

 Siku ya leo ni mwanzo wa Wiki takatifu ambapo Wakristo wanaadhimisha siku tatu kuu za Pasaka yaani Alhamisi Kuu, Ijumaa Kuu na Jumamosi Takatifu.

 Francis alionya dhidi ya hali ya kujihisi mshindi na kuhukumu wengine kama watu duni. Papa amesema aina moja ya hali hiyo ni kujitapa kwa ushindi wa kiroho, ambayo amesema inaashiria kitisho kikubwa kinacholikabili kanisa Katoliki. Francis amependekeza unyenyekevu kuwa njia ya kupambana na hali hilo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.