Header Ads

Paul Scholes matatani kwa kubeti


Mchezaji Mstaafu wa Timu ya Taifa ya England na Klabu ya Manchester United, Paul Scholes atuhumiwa kwa kushiriki kubashiri(betting) matokeo ya michezo ya mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Uingereza(FA), Paul Scholes amejihusisha na 'betting' kwa kipindi cha miaka 4 hadi Januari mwaka huu.

FA imesema Scholes amekiuka kanuni za soka kwani alikuwa akifanya ubashiri huo hata hata wakati alipokuwa mmiliki mwenza wa timu ya Salford City.

Kwa muda wote huo Scholes alishiriki 'betting' mara 140 na endapo atakutwa na hatia atatozwa faini ya zaidi ya Tsh. Milioni 90.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.