Header Ads

Prof Assad Atoa ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka fedha ulioishia 30 juni,2018
Na Jackline Victor kuwanda 
DODOMAl: Imeelezwa kuwa katika mwaka wa fedha mwaka 2017/2018, mamlaka ya mapato Tanzania ilikusanya shilingi trilioni 15.38 ikilinganishwa na malengo yaliyowekwa ya kukusanya shilingi trilioni 17.31 hivyo kuwa na nakisi ya makusanyo kwa shilingi trilioni 1.93 ambazo ni sawa na asilimia 11 ya malengo.

Hayo yamesemwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Pro. Mussa Juma Assad Jijini Dodoma wakati akitoa tarifa kwa vyomba vya habari kuhusu ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 juni ,2018 ambapo amesema kuwa  jumla ya makusanyo hayo haikujumlisha shilingi bilioni 18.95 ambazo ni vocha za misamaha ya kodi kutoka hazina, hivyo makusanyo hali ya mwaka 2017.2018 ni shilingi trilioni 15.40 yakijumuisha na vocha za misamaha ya kodi kutoka hazina.

Aidha, Profesa Assad amesema kuwa mamlaka ya mapato Tanzania ina mashauri ya kodi  ya thamani ya shilingi  trilioni 382.6 kwenye mamlaka za rufaa za kodi ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi trilioni 378.2 ( asilimia  8595).


Mbali na hilo profesa asad amezungumzia matokeo ya ukaguzi wa mashirika ya umaa ambapo amesema kuwa kuwa ukaguzi wa mashirika ya umma ulibaini masuala mbalimbali ambayo serikali inapaswa kuyafanyia kazi ili kuboresha usimamizi wa rasilimali za umma.Hatahivyo, Profesa Asad amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe magufuli kwa ushirikiano wake na kipaumbele alichokitoa wakati wa kupokea ripoti hizo pamoja  na serikali nzima ya awamu ya tano .

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.