Header Ads

Prof Hamis Juma asema mahakama yakakabiliwa na upungufu wa bajeti kwaajili ya vikao vya kusikiliza mashauri


Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema Mahakama inakabiliwa na upungufu wa bajeti kwa ajili ya vikao vya kusikiliza mashauri. Amesema endapo kungekuwa na bajeti ya kutosha vikao vingi zaidi vya mashauri vingefanyika na kumaliza mlundikano wa mashauri ya muda mrefu.

Ameeleza hayo akifungua Mkutano wa mwaka wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wa kutathmini utendaji kazi wa Mahakama hiyo  wa mwaka 2018 na kuweka mikakati ya kazi kwa mwaka 2019.

Alisema sheria imerekebishwa na kuwapa mamlaka Mahakimu na Manaibu Wasajili kusikiliza mashauri ya Mahakama Kuu hususan yale yanayohusu migogoro ya Ardhi ambapo hatua hii itasaidia kupunguza mashauri mahakamani. Aliongeza kuwa ili Mahakama iweze kuwatumia inahitaji kuongezewa bajeti Zaidi ya iliyopo sasa.

Mkutano wa Mwaka huu wa Majaji wa Mahakama ya Rufani pia umewashirikisha Manaibu Wasajili, wasaidizi wa kisheria wa Majaji, Makarani na watunza kumbukumbu ili waweze kusaidiana na Majaji kupanga mikakati ya kumaliza mashauri kwa wakati.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.