Header Ads

Rais wa TFF adaiwa kupokea rushwa kutoka kwa Rais wa CAF


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Wallace Karia anadaiwa kuwa miongoni mwa walionufaika na Tsh. Milioni 46 zilizotolewa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika(CAF), Ahmad Ahmad zinazoelezwa kuwa ni rushwa.

Rais Ahmad anatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi, ikiwa ni miaka miwili tu tangu alipotwaa uongozi wa Shirikisho hilo la soka.

Nyaraka zilizowasilishwa FIFA zimeonesha kuwa Ahmad Ahmad aliisababishia CAF hasara ya takribani Tsh. Bilioni 2 kwa kuagiza vifaa kupitia kampuni ya Ufaransa ijulikanayo kama Tactical Steel.

Pia, anatuhumiwa kuwadhalilisha watumishi wanne wa kike wa CAF ambao majina yao yameifadhiwa pamoja na kukiuka sheria za CAF kwa kuongeza uwakilishi wa Morocco ndani ya shirikisho hilo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.