Header Ads

Ripoti: Adhabu ya kifo yapungua kwa kiasi duniani


Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limebaini kwamba adhabu ya kifo ilipungua kwa asilimia kubwa mnamo mwaka 2018.

Katika ripoti yake shirika hilo limesema kuwa mnamo mwaka 2018 liliorodhesha angalau watu 690 walionyongwa katika nchi 20, ikiwa ni sawa na chini ya asilimia 31 ikilinganishwa na mwaka 2017, kiwango cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa, kulingana na ripoti ya Aprili 10, 2019.

Watu wengi walinyongwa nchini China, Iran, Saudi Arabia, Vietnam na Iraq. Idadi hiyo inaweza kuwa kubwa nchini China, limebaini shirika hilo.

Mbali na China, nchi nne zinachukua asilimia 78 ya watu walionyongwa duniani kote: Iran, Saudi Arabia, Vietnam na Iraq. Hata hivyo, Iraq, Pakistan na Somalia pia zinaonyesha kuwa utekelezaji wa adhabu ya kifo umepungua kwa kiasi kikubwa kwa mwaka 2018.

Hata hivyo baadhi ya nchi, kama vile Belarus, Marekani, Japan, Singapore na Sudan Kusini wametekeleza adhabu ya kifo na kuua watu wengi, imesema Amnesty International.

Thailand imetekeleza adhabu hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009. Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena, hivi karibuni alisema anataka kurejelea adhabu ya kifo baada ya kusitishwa kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita, Amnesty International imeongeza.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.