Header Ads

Serikali kuwalipa waliohasiwa kwa nguvu Japan


Maelfu ya raia ambao walihasiwa bila ridhaa Japan wameombwa radhi na serikali na wanatarajiwa kulipwa fidia.

Chini ya Sheria ya Kulinda Vizazi ambayo ilitekelezwa na mamlaka nchini humo kwa takribani miongo mitano, maelfu ya watu walihasiwa ili kuzuia kuzaa watoto ambao 'wangelikuwa dhaifu'.

Sheria hiyo ilitumika kwa miaka 48, kuanzia 1948 mpaka 1996, na iliwalenga watu ambao walikuwa na ulemavu wa viungo, akili, na matatizo ya kitabia.

Waziri Mkuu wa Japani, Shinzo Abe ameomba radhi kwa "maumivu makali" ambayo wameyapitia.

Chini ya sheri mpya ambayo imesainiwa leo Jumatano, Aprili 24 wahanga wote ambao wapo hai watalipwa yen milioni 3.2 sawa na dola 22,000.

Wengi wa wahanga waliohai kwa sasa walikuwa watoto wakati walipofanyiwa upaasuaji wa kuhasiwa.

Mtu aliyehasiwa anakosa uwezo wa kupata watoto.

Wahanga hao sasa wanatakiwa kuomba malipo ya fidia ndani ya kipindi cha miaka mitano. Maombi yao yatapitiwa na bodi ya wataalamu kabla ya kulipwa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.