Header Ads

Serikali yafanya jitihada hizi ili kupunguza ajali za barabarani nchini


Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  imeendelea kupunguza ajali za barabarani kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani zinazofanywa na wadau wa usalama barabarani.


Akizungumza  leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati ya Bloomberg Deus Sokoni alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendeea kutoa elimu kwa umma pamoja na uboreshaji wa miundombinu ili kupunguza ajali na vifo kwa watanzania.

Mrakibu Msaidizi wa huyo wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati ya Bloomberg Sokoni alisema “Barabara nyingi zinazojengwa hivi karibuni zimekuwa zikizingatia viwango vya ubora vyenye kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa barabara ikiwemo watembea kwa miguu”

Alifafanua zaidi kuwa siku za nyuma barabara hazikuwa zikijengwa kwa ubora wa kuzingatia watumiaji wote wa barabara mfano wa barabara ya Dar es salaam iliyopo jijini Dodoma, ambayo imesababisha ajali mara kadhaa.

Aidha, Mrakibu Msaidizi huyo wa Polisi ametaja jitihada nyingine za Serikali za kupunguza ajali ni pamoja na ujenzi wa barabara za mzunguko na mchepuko ambazo zinasaidia kuondoa msongamano wa foleni katika majiji mbalimbali nchini.

Baadhi ya miradi ya Serikali inayoendelea kutekelezwa kwa lengo la kupunguza ajali na foleni nchini ni pamoja na ujenzi wa  barabara  za mzunguko ndani ya Dodoma  yenye urefu wa kilomita 39 pamoja  na barabara za mchepuko zinazojengwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Naye, Mwendesha pikipiki wa jijini Dodoma Amos Majenda alisema kuwa Serikali imesaidia kupunguza ajali kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani ambayo inawafikia watumiaji wengi wa barabara.

Majenda alisema “Serikali imejitahidi kutoa elimu si kama kipindi cha nyumba ambapo ajali zilikuwa nyingi zaidi, ajali zinazotokea hivi sasa ni kwa sababu watu hawazingatii sheria za usalama barabarani na hivyo madereva wanaendesha vyombo vya moto kwa mwendokasi na kutovaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria”

Mafunzo hayo yanayotolewa kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani nchini yana lengo la kuwajengea uwezo waaandishi wa habari ili waweze kusaidia kufikisha elimu kwa umma, sambamba na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kutatua changamoto za ajali za barabarani nchini.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.