Header Ads

Simba SC U20 na Cameroon U17 wavimbiana


Timu ya vijana, Simba SC U20 imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Taifa ya Cameroon U-17 katika mchezo wa kirafiki ambao umepigwa kwenye viwanja vya JK Youth Park.

Timu ya Taifa ya Cameroon U-17 ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza fainali za AFCON U17 zitakazoanza April 14 mwaka huu,na Tanzania ndio mwenyeji wa fainali hizo.

Hii imekuja baada ya Uongozi wa Klabu ya Simba SC kukubali ombi la Shirikisho la mpira wa miguu la nchini Cameroon la kuomba kucheza mchezo huo. Lengo la Shirikisho hilo kuomba mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi kwao ya kucheza fainali hizo za AFCON U17

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.