Header Ads

Sisitizo la Kiongozi wa Korea Kaskazini la udharura wa kubadilishwa siasa za Marekani kuihusu Pyongyang


Kiongozi huyo amesema kuwa, ili kuendelea mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Washington, inatakiwa kwanza ibadili siasa zake kuihusu nchi hiyo. Kim Jong-un ameongeza kwamba kushindwa mazungumzo na Marekani, kuna maana ya kuongezeka mizozo katika eneo la Rasi ya Korea.

 Amesema kuwa, hatopendelea kukutana na Rais Donald Trump wa Marekani, iwapo rais huyo hatofuata mwelekeo sahihi. Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini pia ameipa Marekani muda wa hadi mwishoni mwa mwaka huu (2019), iwe imechukua hatua madhubuti kwa ajili ya kubadilisha mazingira ya sasa sambamba na kufuata mwelekeo mpya kuihusu Pyongyang. Onyo la Kim Jong-un kwa Marekani juu ya udharura wa kubadilishwa siasa za nchi hiyo kuihusu Pyongyang, imetolewa baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kusisitiza kwenye kikao chake na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kwamba ataendelea kuiwekea vikwazo serikali ya Pyongyang.

Trump ametangaza msimamo huo, katika hali ambayo, Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini alikuwa amefanya safari nchini Marekani kwa ajili ya kumshawishi rais huyo wa Marekani kuiondolea Pyongyang baadhi ya vikwazo, suala ambalo hata hivyo halikufikiwa katika safari yake hiyo.

Kuendelea misimamo ya uhasama ya Trump dhidi ya nchi hiyo ya Asia, kunajiri katika ambayo ilitazamiwa kuwa baada ya Washonton na Pyongyang kukubaliana kuendelea na mazungumzo yao, White House ingeiondolea baadhi ya vikwazo Korea Kaskazini kwa ajili ya kuleta hali ya kuaminiana na kwa ajili ya kuyafanya mazungumzo hayo yaweze kupiga hatua zaidi mbele.

Siasa hizo za Rais Donald Trump za kupenda makubwa dhidi ya Korea Kaskazini ndizo zilipelekea kuvunjika duru ya pili ya mazungumzo kati ya Washington na Pyongyang nchini Singapore na Vietnam, licha ya kwamba Korea Kaskazini ilikuwa imeahidi kusimamisha majaribio yake ya silaha za nyuklia na makombora ya balestiki. Kwa kuzingatia siasa za vitisho na vikwazo dhidi ya nchi hiyo

ya Asia, tangu kulipoanza mazungumzo ya nchi mbili hapo mwezi Juni mwaka jana nchini Singapore hadi sasa, na hasa kwa kuwa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa ulifanywa na Pyongyang pakee, hivyo muhusika mkuu wa kuvunjika mazungumzo na kuendelea mgogoro wa Rasi ya Korea ni rais huyo wa Marekani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.