Header Ads

Taasisi ya CODO yafanya kongamano Jijini DodomaDODOMA:Taasisi isiyo ya kiserikali CODO inayoshughulika na kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu imefanya kongamano Jijini Dodoma na vyombo vya habari katika kujadili  changamoto wanazo kumbana nazo ili kuwa na taifa lisilo tegemezi

Mwenyekiti wa taasisi ya CODO Jackson Misiga amesema kuwa lengo la kuanzisha taasisi hiyo kutokana na baadhi ya jamii kuishi katika mazingira magumu na kuona kuwa kuna umuhimu  mkubwa kusaidia jaamii katika Afya,Elimu na uchumi ambapo ameeleza utofauti wa taasisi hiyo na Taasisi nyingine.Aidha Misiga ameongeza kuwa wana hudumia watoto 47 ambapo watoto 10 wapo vyuoni na wengine wapo sekondari na kueleza kuwa watoto wote watakatiwa Bima ya Afya.

Aidha Noel Nguzo Afisa miradi Taasisi ya CODO amesema kuwa wanahitaji fedha kiasi cha shilingi milioni 120 ili waweze kuongeza idadi ya watoto 2000 ambapo watoto 500 watapata  Bima ya Afya,huku akisema kuwa tarehe 8 mei 2019 watatembelea shule za sekondari na shule za Msingi za mainispaa ya Dodoma ili kuongea na watoto pamoja na wazazi kujua hali ya maisha yao.


Hata hivyo miongoni mwa washiriki wa mdahalo huo ameshukuru vyombo vya habari kushiriki kongamano hilo huku akieleza mafanikio walio yafanya kusaidia watoto wanao ishi katika mazingira magumu.
Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.