Header Ads

TAKUKURU YABAINI UPUNGUFU KATIKA UJENZI WA MIRADI YA HOSPITALI WILAYA ZA KYERWA


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera imebaini upungufu katika ujenzi wa miradi ya hospitali za wilaya ya kyerwa, Bukoba na karagwe ambapo miradi hiyo inagharimu sh billion moja na million mia tano kwa kila mradi.

Haya yameelezwa na Kaimu wa Afisa TAKUKURU mkoa wa Kagera, Bi. Siaba Omary wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mwaka wa fedha wa 2018/2019 kuanzia Januari mosi hadi Machi mwaka huu.

"Tumebaini fedha za miradi hiyo kutumika vibaya tofauti na kazi nyingine ya majengo saba yaliyokusudiwa na kwa kila wilaya, mfano kuajiri walinzi na kujenga majengo ya stoo. Muundo wa kamati ya ujenzi kwa baadhi ya wilaya haukufata taratibu zinazotakiwa mfano mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kuwa Afisa ugavi badala ya mhandisi wa wilaya. Malipo ya mafundi kucheleweshwa. Baadhi ya wilaya kutoendana na wakati pamoja na serikali kutoa fedha hizo na kutoa muda maalumu wa kuyakamilisha na kuna baadhi ya wilaya ndio kwanza majengo hayo yapo katika hatua ya msingi" Alisema bi Siaba Omary.

Aidha amesema kuwa takukuru mkoa Kagera imepokea malalamiko 188 kuanzia Januari 2019 mpaka March 2019 ambapo amesema kuwa maeneo sita yamelalamikiwa sana,"
"Maeneo yaliyolalamikiwa sana ni pamoja ni Tamisemi, Mahakama, Polisi, Ardhi, Mifuko ya hifadhi ya jamii na Elimu" ambapo amewataka viongozi wa sekta hizo kutathimini mwenendo wa watumishi walio chini yao na kiwango cha huduma wanayoitoa kwa jamii.

Aidha TAKUKURUimebaini ukiukwaji mkubwa katika uendeshaji wa baraza la kata hususani katika kipengere cha gharama za ufunguaji mashauri, kutembelea maeneo ambayo halmashauri imetenga kiwango lakini mabaraza mengi yamekuwa yakipanga bajeti zake pamoja na gharama za kupata nakala ya hukumu

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.