Header Ads

TAKUKURU yambana mbavu mwalimu aliyetumia madaraka yake vibaya


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Tanga, Iimemtaka mwalimu mstaafu aliyetumia madaraka yake vibaya na kuliingizia taifa hasara ya Sh. Milion 30 ambazo zimetokana na kulipwa mshahara kwa kipindi cha miezi 31 wakati ameshaandika barua ya kuomba kustaafu na amekubaliwa, kuonana na uongozi huo ili kutafuta njia sahihi ya kulipa deni hilo na endapo atashindwa TAKUKURU itauza nyumba yake ili kufidia deni hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mstaafu aliyejulikana kwa jina la Aneth Makame mkazi wa wilayani Muheza mkoani Tanga shauri lake kufika mwisho wa kutolewa maamuzi ikiwa ni kati ya mashauri 25 yaliyoendeshwa na TAKUKURU kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.