Header Ads

TAKUKURU yamfikisha Mahakamani kigogo mwingine


Mfanyabiashara, Florencia Mashauri - Mkurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil and Gas Limited watafikishwa Mahakamani leo na TAKUKURU kwa kujibu mashtaka ya wizi, uhujumu uchumi, ukiukwaji wa sheria ya mafuta juu ya ujengaji wa kituo cha uuzaji wa mafuta kwa UDART pamoja na makosa ya utakatishaji wa fedha haramu ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.2.

Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa Februari 11 mwaka huu iliwafikisha mahakamani watuhumiwa wanne katika kesi ya uhujumu uchumi namba 11.

Kesi hiyo inawahusu viongozi wa shirika la usafirishaji Dar Es Salaam  - UDART pamoja na wafanyabiashara ambao walishtakiwa kwa makosa ya wizi, kughushi pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.

Hayo yamezungumzwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi TAKUKURU, Kassim Ephrem katika Mkutano wake na waandishi wa habari.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.