Header Ads

TAWCA wakumbushwa uthubutu kujiamini na aliyekuwa Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda


Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akikabidhiwa vipeperushi vya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) baada ya kufunga mkutano wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini(TAWCA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.TANESCO ndio waliofanikisha kufanyika kwa mkutano huo kwa kuamini utaleta tija katika maendeleo ya nchi hasa kwa kuzingatia ulilenga kuwajengea uwezo wanawake wahasibu


SPIKA wa Bunge mstaafu Anne Makinda amewataka Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini( TAWCA)kujiamini,kuthubutu na kuwa na mtandao katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendelo nchini.

Pia amewakumbusha TAWCA wahakikishe wanawajali wanawake wa hali chini kwa kuwajali na kuwasaidia kufanikisha ndoto zao pamoja na kuwaonesha upendo.

Makinda ameyasema hayo wakati anafunga Mkutano wa Pili wa TAWCA ambapo mkutano huo umefanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam .Wahasibu wanawake wa TAWCA wameshiriki mkutano huo.

"Niwapongeze sana TAWCA kwa namna ambavyo mmejadili mambo yenu na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo mlipokuwa kwenye mkutano wenu kupitia mada ambazo zimetolewa.Kwa namna ambavyo mmejipanga na kwa mikakati yenu mtafika mbali sana.Ni wanawake wenye utalaam wenu ambao mnapanga mambo yenu na yanapangika.Hongereni sana," amesema.

"Hakikisheni suala la muda mnalipa kipaumbele kinyume na hapo mambo hayatakwenda sawasawa.Muda ni muhimu katika kupanga maendeleo,pia tengenezeni mtandao ambao nao ni muhimu kwani huwezi kufanya maendeleo peke yako," amesema Makinda.

Kuhusu TAWCA kuwajali wanawake wengine na hasa wale wanaonekana wa hali chini,Mama Makinda amesema ni muhimu wanawake wa chini wakaoneshwa upendo kwani humsaidia kumpa faraja na kubwa zaidi kuhakikisha wanabeba ndoto zao na kuzifanyia kazi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.