Header Ads

Ubabe wa Nigeria kwa soka la vijana


Timu ya taifa ya Nigeria chini ya miaka 17 maarufu kama Golden Eagles ama 'Kinda la Tai' ilitwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 1985 nchini China, mashindano hayo ya mwaka 1985 yalidhaminiwa na KODAC kipindi hicho michuano hiyo inahusisha vijana chini ya miaka 16.

Walitwaa taji la vijana mwaka 1993, 2007, 2013 pamoja na 2015 na kuwa timu ya pili baada ya Brazil kutwaa mara mbili mfululizo.

Pia Kinda hilo la Tai ndio timu pekee ya vijana kutwaa mataji matano ya kombe la dunia, Nigeria pia imetwaa taji la AFCON chini ya miaka 17 mwaka 2001 pamoja na mwaka 2007 ikishika nafasi ya pili mwaka 1995.

Baada ya kutwaa taji mwaka 2007 kulizuka majadiliano kwenye timu hiyo ya vijana wakitaka walipwe fedha au wapewe vitega uchumi, waliingia kwenye michuano ya kombe la dunia la FIFA la chini ya miaka 17 la mwaka 2009 wakiwa chini ya kocha Henry Nwosu ambaye nafasi yake ilikuja kuchukuliwa na kocha John Obuh kocha wa Kwara United.

Pamoja na yote Nigeria ilishindwa kufuzu kombe la dunia chini ya miaka 17 mwaka 2011 ingawa walirejea mwaka 2013 lakini mipango yao ilivurugwa mwezi August ambapo wachezaji muhimu walikamatwa kwenye vipimo vya MRI.

Kwenye mchezo wa kwanza waliwafunga mabingwa watetezi Mexico mabao 6-1 walishindwa kuifunga Sweden tu kwenye hatua ya makundi ingawa hilo liliwezekana kwenye hatua ya nusu fainali . Kwenye mchezo wa fainali walikutana na Mexico na kufanikiwa kuifunga kwa mara ya pili na kutwaa taji la kombe la dunia chini ya miaka 17 kwa mara nyingi zaidi.

Timu hii pia ilikumbwa na mkasa wa udanganyifu kwa mara nyingine, miongoni mwa wachezaji 26 waliopimwa nusu yao walijikuta wamefeli kipimo cha MRI mwaka 2016.

Katika michuano ya mwaka huu iliyoanza jana April 14, 2019 hapa Tanzania, Nigeria wapo Kundi A pamoja na wenyeji Tanzania 'Serengeti Boys', Uganda na Angola.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.