Header Ads

Waandamanaji Sudani kuendelea na maandamano


Waandamanaji nchini Sudani wameapa kuendelea na maandamano saa chache baada ya jeshi kuchukuwa hatua ya kumtimua rais Omar al-Bashir kwenye wadhifa wake na kuchukuwa madaraka.
Rais Omar al-Bashir alipinduliwa na kukamatwa siku ya Alhamisi baada ya miezi kadhaa ya maandamano.

Waandamanaji wameliita Baraza la jeshi kuwa ni muendelezo wa utawala ulio kuwepo na kusema kuwa wataendelea kupambana na kupinga kwa amani.

Hata hivyo taarifa rasmi iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali vilisema kuwa tahadhari ya kutotoka nje itaanza kutekelezwa kuanzia saa nne za usiku siku ya Alhamisi Aprili 11 majira ya Sudan.

Waziri wa Ulinzi Awad Ibnouf amesema, jeshi litaongoza kwa kipindi cha mpito, kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi mpya na kupatikana kwa Katiba mpya.

Wakati huo huo Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Uingereza wamelaani jaribio la mapinduzi nchini Sudani wakisema kuwa Omar al-Bashir na serikali yake wamechaguliwa kidemokrasia, na hivyo kulitaka Baraza la jeshi kukabidhi madaraka kwa raia haraka iwezekanavyo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.