Header Ads

Wadau wa michezo watakiwa kujitokeza kuendeleza mchezo wa volley ball
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayuob Mohammed Mahmoud, amewataka wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa pamoja na kuendeleza Mchezo wa Volley ball kutokana na Mchezo huo kuonekana kuwa nyuma.

Hayo aliyabainisha wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Michezo wa Mpira wa WAVU (volley ball day) lilofanyika katika Viwanja vya timu ya Mafunzo Kilimani Mjini Magharib Unguja, Alisema bado jitihada za pamoja zinahitajika katika kukuza michezo husani mchezo wa Volley ball.

Rc Ayoub alisema kuwa jitihada za pamoja zinahitajika kati ya serikali na wadau mbali mbali katika kukuza mchezo nchini, alisema Michezo ikiendelezwa inaleta urafiki na udugu ambapo hapo awali haukuwepo baina yao wanamichezo.

Aidha alisema kuwa rais Dk. Shein mara tu baada ya kuingia madarakani alidhamiria kuendeleza michezo nchini jambo ambalo linapaswa kuungwa mkono na kila mmoja wao.

Hivyo kitendo cha timu ya Mafunzo kuandaa Tamasha hilo la Michezo linaashiria wazi kuunga mkono juhudi za rais pamoja na kutekeleza Sera ya Serikali ya kuimarisha michezo katika taasisi zote za Serikali.

Katika hafla hiyo Ayoub aliahidi kutoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kuendelea kufanyiwa matengenezo kiwanja hicho cha Mafunzo ambapo alisema kuwa kumalizika kwake kutaweza kuwasaidia wanamichezo wengi wa mchezo huo hapa nchini.

Pia  aliahidi kutoa shilingi 100,000 kwa timu zote zilizoshiriki tamasha hilo ambalo lina lengo la kuhamasisha watu kushiriki mchezo huo.

Nae Kamishna wa Mafunzo Zanzibar Haji Hamdu alisema lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kutoa fursa kwa vijana kushiriki katika michezo.

“Huwa tunaandaa Matamasha mbalimbali tukiwa na lengo kuwavutia vijana kushiriki michezo kwani tuna amini Michezo ni Umoja huleta udugu na umoja baina yetu” alisema Kamishna wa Chuo cha Mafunzo.

Mapema naibu Kamishna wa Vyuo Vya Mafunzo Zanzibar Haji Hamdu, alisema kuwa lengo la kufanyika kwa tamasha hilo ni kuhakikisha wanatoa hamasa kwa vijana kujiunga katika  mchezo huo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.