Header Ads

Wanafunzi wa Ngomeni Tanga wajisaidia porini


Wanafunzi shule ya sekondari Ngomeni iliyopo kata ya Ngomeni wilayani Muheza Mkoani Tanga wanajisaidia porini kutokana na ukosefu wa vyoo.

Mwenyekiti wa kamati ya shule ya sekondari Ngomeni Kamba Mkiwa Ramadhani amesema hali itakuwa mbaya zaidi endapo hakutajengwa vyoo baada ya likizo fupi ya mwezi wa nne  .

Afisa elimu sekondari ngazi ya wilaya Julita Akko amehoji kwa viongozi wa shule na kata kuwa iweje mfuko wa jimbo umechangia mifuko ya saruji 20 pamoja na mabati lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo ameagiza ujenzi uanze mara moja huku mganga mkuu wa wilaya akisistiza kuwa endapo agizo hilo halitatekelezwa shule itafungwa kwa mujibu wa sheria.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.