Header Ads

Wanaotaka kuandamana waonywa


Mkuu wa jeshi la Polisi ,Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro ameonywa wale watakaoandamana bila ya kuwa na kibali watakuwa wanatenda uhalifu.

IGP Sirro amesema tayari ameshatoa maelekezo kama maandamano ni halali hana shida ila kama ni kinyume na hapo shida itakuwepo kwa yule atakayeandamana.

”Kwa sababu kama unaandamana maandamano sio ya halali ni uhalifu na utapambana na polisi, kama ni halali taratibu zipo kama barua ipo na mmekubaliana kwamba unaendelea na tutakulinda hamna shida. Lakini kama hujaleta barua ya kutupa taarifa kuwa utafanya maandamano na ukafanya unaingia kwenye uhalifu," amesema IGP Sirro.

”Niwaombe si wakati wa kutaka kujiingiza kwenye uhalifu pasipokuwa na sababu, fuata taratibu, mwishowe utaona jeshi la polisi baya wakati ni lakwenu, haskari hawa ni wakenu, ukienda Kigoma, Kagera, Geita ndiyo utaona jinsi gani askari wanafamnya kazi.” amesisitiza.

IGP Sirro ametoa onyo hilo wakati kukiwa na taarifa kwenye mitandao kijamii juu ya kufanyika kwa maandamano ya amani mkoani Dodoma yanayoratibiwa na kijana kutoka Chama cha ACT-Wazalendo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.