Header Ads

Wanaotangaza maandamano kwa njia ya mtandao ,wakiingia barabarani watapigwa watachakaa-Muroto

Na Jackline Victor Kuwanda 
DODOMA:Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limewatahadharisha wananchi kuepuka kujiingiza katika mkumbo wa uhamasishaji  maandamano  kwani wasije wakaingia katika mikono ya serikali kutokana na kuvunja sheria za nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema kuwa kuna taarifa zilizolifikia jeshi hilo  kuwa kuna vijana wa chama cha ACT WAZALENDO kwa kushirkiana na vyama vingine vya siasa vikiwemo vya NCCR MAGEUZI,CHAUMA,UPDP na vyama vingine vitatu ambavyo wanavijua wao.

'' wanatarajia kufanya maandamano  siku ya jumanne tarehe 9/4/2019  waliyoyapa jinakuwa maandamano  ya amani  wakiwa na lengo la kulishinikiza bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kutekeleza kumshinikiza spia wa bunge kufuta azimio la Bunge la kutofanya kazi na CAG Pro Musa .J. Assad'' Muroto 


Aidha, ameongeza kuwa kutokana na taarifa walizo nazo pamoja na taarifa zilizosambaa mtandaoni, jeshi la polisi mkani hapa linapiga marufuku maandamano hayo  kufanyika kwani  hayatakuwa maandamano halali kwa kuwa hayana kibali.

Pia , amesema watambue kuwa  Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni mhimili unaojitegemea na hautakiwa kuhojiwa nje ya Bunge kwani wanaohoji mipango na maazimio ya bunge wamo ndani ya bunge ambao ni wabunge wenyewe walioteuliwa na wananchi  ili kuwawakilisha.


Hatahivyo jeshi hilo limewaondoa wasiwasi rais wema ambao wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kiuchumi jijini hapa na waendelee na shughuli zao kama kawaida kwani jeshi la polisi mkoa wa Dodoma litaendelea kuwalinda na kuhakikisha hawabaguliwa katika kazi zao ili kuanya Dodoma kuendelea kuwa sehemu salama.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.