Header Ads

Watanzania waaswa kujitokeza kusajili laini kwa njia ya vidole
DODOMA: Watanzania wameaswa kujitokeza kusajili laini kwa njia ya vidole ili kepuka changamoto za  mitandaoni kama wizi,na Maneno yasiyofaa yanayo andikwa mtandaoni.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya miaka kumi ya Mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF jijini Dodoma,na maonyesho hayo yameambatana na kauli mbiu isemayo  ‘mawasiliano kwa wote ni kichocheo uchumi wa kati’ambapo amesema mfuko wa mawasiliano umesaidia kwa kiasi kikubwa kupeleka mawasiliano sehemu mbalimbali hadi kufika asilimia 94%  ya wananchi  kupata mawasiliano.

Aidha nditiye ameyapongeza  makampuni ya simu Tanzania  kwa kuonyesha mshikamano katika mfumo wa usajili laini kwa vidole ambao utaanza mei 1 2019 hadi December 31 2019 huku akiwataka watu kusajili laini moja kwa kila mtandano.


kwa upande wake mdauwa mawasiliano ambaye ni Meneja wa Tigo Pesa na usambazaji mkoani Dodoma Gidion Moris amesema kuwa mfumo wa kusajili laini kwa vidole ulianza toka mwaka 2018 kwa ofisi zote za Tigo kwa watu ambao wana vitambulisho vya Taifa huku akiwataka wateja wa laini za tigo kujitokeza kusajili laini kwa mfumo wa vidole ambapo kila mtu atasajili laini moja.


Naye Emmanuel John Medukenya ambaye ni mfanyakazi wa mtandao wa Vodacom amesema kuwa mfumo huo ni mzuri kwa watumiaji wa mitandao nchini huku akieleza  umuhimu wa kusajili laini kwa vidole kuwa utasaidia kuepuka wizi wa mtandaoni sambamba na kutoa wito kwa watumiaji wa laini za Vodacom.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.