Header Ads

Watu 150 wahofiwa kufa baada bodi kuzama


Takribani watu 150 hawajulikani walipo na kuhofiwa kupoteza maisha nchini DR Congo  baada ya kuwepo na taarifa jana jioni za kuzama kwa boti katika ziwa Kivu mashariki mwa mchi.

Rais Felix Tshisekedi aliandika katika ukurasa wa Twita kuwa anasikitishwa na kuzama kwa boti kwenye ziwa Kivu na kutoa pole kwa familia. Hadi sasa watu watatu ndio waliothibitishwa kupoteza maisha.

Kwa upande wake Waziri wa usafiri wa mkoa Jaqcueline Ngengele amelieleza shirika la habari la dpa, kuwa kati ya abiria wanaokadiriwa kufikia 200 ni abiria 40 tu ambao wameokolewa. Waziri huyo amesema hali mbaya ya hewa na kujaza kupita uwezo vimechangia ajali.

Hata hivyo, Afisa mwingine wa mkoa amesema abiria wengi hawakuwa wamevaa majaketi ya kujiokoa. Ajali za kuzama kwa boti zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika maziwa na mito nchini Congo. Mwaka 2001 watu kati 100 hadi 150 walifariki baada ya boti kuzama katika ziwa Kivu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.