Header Ads

Waziri makamba atoa neno kuhusu mifuko ya plastikiDODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira JANUARY MAKAMBA  amesema inawezekana Julai mosi mwaka huu ikawa ndio mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Tayari kanuni za utekelezaji wa sheria ya kuzuia matumizi ya  mifuko hiyo zipo tayari zinasubiri kutangazwa kwenye gazeti la serikali.

Waziri MAKAMBA amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Kaliua MAGDALENA SAKAYA aliyetaka kujua kama serikali haioni kuwa inaendelea kulinda matumizi ya mifuko hiyo.

Awali katika swali la msingi mbunge huyo ametaka kujua serikali ina mikakati gani ya kuondoa matumizi ya plastick hapa nchini.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa wizara hiyo MUSSA SIMA amekiri kuwa ni kweli matumizi ya mifuko hiyo imeongezeka hasa kutokana na mifuko hiyo kutolewa bure kwenye maduka,masoko,migahawa na maeneo mbalimbali.


Amehimiza viwanda vinavyozalisha mifuko ya plastiki na wadau wengine kujitayarisha kwak ubadili teknolojia na kuthamini fursa zinazojitokeza katikak uzalisha mifuko mbadala hasa katika kipindi hiki cha mpito wakati taratibu za maamuzi ya serikali zikikamilishwa..

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.