Header Ads

Waziri mwakyembe awatoa hofu watengenezaji wa filamu


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amewatoa wasiwasi watengenezaji wa filamu ambao wanataka kutengeneza filamu kumuhusu Rais wa nchi.

Akizungumza kwenye kongamano la waigizaji lililoandaliwa na Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na Chama cha Waigizaji Taifa amesema waandaaji wa filamu wanaruhisiwa kumuigiza Rais ni lazima bajeti ya filamu hiyo iwe inaendana na hadhi ya uongozi huo mkubwa wa nchi.

‘’Hivi inawezekana Rais wa nchi  unamwigiza anatoka kwenye vile vigari vi-scopio anatoka amejikunja, nchi gani hiyo? sisi hatuna Rais wa namna hiyo. Hii nchi ini uwezo, Rais gani hata gari nzuri hana," alihoji.

"Ukitaka kumuigiza Rais hakuna anayekuzuia lakini muswada wako ubebe ile Heshima ya uongozi wa juu wanchi kama wenzetu wanavyobeba heshima ya uongozi wao," alieleza.

Aidha Waziri Mwakyembe awewataka waandaaji wa filamu kuwasilisha mapendekezo yao wizarani ili waweze kupata msaada wa kutumia sehemu zenye uhalisia kama kambi za jeshi, vituo vya Polisi na maeneo mengine.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.