Header Ads

Waziri Netanyahu aelekea kushinda uchaguzi wa Israel


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mpinzani wake mkuu Benny Gantz wamedai kupata ushindi katika uchaguzi wa hapo jana lakini matokeo ya mwanzo yanaashiria kuwa kiongozi huyo mkongwe wa siasa za mrengo wa kulia anaelekea kushinda muhula wa tano.

Huku asilimia 80 ya kura zikiwa zimeshahesabiwa matokeo ya mwanzo yanaonyesha kuwa Chama cha Netanyahu cha Likud kimepata viti 38, wakati Gantz wa chama cha siasa za wastani cha Bluu na Nyeupe kikiwa na viti 36.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa ifikapo Ijumaa, lakini maafisa wa uchaguzi watakuwa wakitoa maelezo kadri hesabu za kura zitakavyokuwa zikikamilishwa. Kama atashinda, Netanyahu mwenye umri wa miaka 69, atakuwa waziri mkuu aliyehudumu kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya Israel ya miaka 71.

Amesema tayari ameanzisha mazungumzo na washirika anaoweza kushirikiana nao katika kuunda serikali ya muungano

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.