Header Ads

Waziri ummy akabidhi vyandarua vyenye dawa viwatilifu kwaajili ya kuwakinga wakina mama wajawazito pamoja na watoto
Na Jackline Victor kuwanda 
DODOMA: Katika Kuelekea  Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo huadhimishwa Aprili 25 ya kila mwaka , Waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto, Mh Ummy Mwalimu  amesema kuwa ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa wanatenga bajeti au fungu maalumu  kwaajili ya kutekeleza mikakati mbalimbali ya kupamba na malaria.

Waziri ummy ameyasema hayo leo  jijini Dodoma katika kituo cha afya cha makole kilichopo Jijini hapa  wakati akikabidhi vyandarua vyenye dawa viwatifulu kwajili ya kuwakinga wakina mama wajawazito pamoja watoto dhidi ya ugonjwa wa malaria huku kauli mbiu ya mwaka huu ikisema ‘’ Zero Malaria inaanza na Mimi’’.


Aidha, waziri  ummy amesema kuwa kati magonjwa ambayo yanaongoza  kuua watanzania ni ugonjwa wa malaria lakini  habari njema ni kwamba toka serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe magufuli  iingie madarakani wameweza kutekeleza mikakati mbalimbali ya kutokomeza  malaria nchini Tanzania.


Mbali na hilo amesema kuwa wakina mama wajawazito wanatakiwa kuhudhuria kliniki mara tu wanapo gundua kuwa ni wajawazito.


Kwa upande wake Fransis Bujiku   ambaye pia Kaimu Mganga  Mkuu wa Mkoa  lakini pia anaratibu kitendo cha udhibiti wa Malaria mkoa wa Dodoma  , amesema kuwa kwa mwaka 2015 kulikuwa na kiwango cha maambukizi kwa asilimia moja  na kwa  kiwango hicho wameweza kukishusha mpaka asilimia 0.6 hivyo ni mafaniko makubwa.


Akizungumza kwa nia ya wakina mama waliopokea msaada huo , ameishukuru wizara ya afya kwa kuwapatia vyandarua hivyo kwani vitawasaidia katika kujikinga na ugonjwa wa malaria pamoja na kutoa ushauri kwa  wakina  mama wenzake kuwa na tabia ya kuhudhuria kliniki.


Hatahivyo , waziri ummy amesema kuwa wana mikakati mbalimbali wanayo itekeleza kama serikali kupitia wizara ya afya kwaajili ya kutokomeza malaria.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.