Header Ads

wenyetabia ya kuiba mifugo kukiona


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP )Saimon Sirro amemtaka Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro (SACP) Wilbroad Mutafungwa kuwakamata na kuwachukulia  hatua watu wenye tabia ya kuiba Mifugo katika wilaya ya Mvomero ili kukomesha tabia hiyo.

Amesema kuna watu wanatabia ya kuiba Ng'ombe na Mbuzi za wafugaji tabia hiyo sio nzuri kabisa jambo ambalo linasababisha uhasama katika jamii ambapo ameagiza wachukuliwe hatua kali za kisheria pindi watakapobainika

IGP Sirro ametoa agizo hilo Mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za askari  polisi katika eneo la Mvomero  na kupata malamiko kutoka kwa wafugaji  kuhusu vitendo vya wizi wa mifugo.

Katika hatua nyingine, IGP Siro  ametembela nyumba kumi za polisi zinazojengwa  Manispaa ya morogoro  na kuahidi kutoa  shilingi milioni kumi kwa ajli ya  kukamilisha ujenzi wa nyumba kumi  za askari polisi ambazo zinajengwa kwa  michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (SACP ) Wilbroad Mutafungwa amesema  Halmashauri ya wilaya  ya Mvomero imejitolea kujenga nyumba nne  za polisi katika wilaya hiyo huku  mwenyekiti wa kamati  ya ujenzi  wa nyumba za Polisi Morogoro B w. Omary Alsaid  amesema  nyumba hizo zinatarajiwa kukamilika kabla ya Mei 30 Mwaka huu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.