Header Ads

wiki kesho tutaanza ziara maeneo yote ambayo yanaonekana kero na changamoto kubwa kwenye sekta ya ardhi-Kunambi
Na Jackline Victor Kuwanda 
DODOMA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Jiji la Dodoma Bwana Godwini kunambi  amesema kuwa kuna changamoto mbalimbali  kwenye sekta ya ardhi, hivyo wataanza ziara kakika maeneo yote ambayo yanaonekana ni kero na changamoto kubwa kwenye sekta  hiyo.

Kunambi ameyasema  hayo leo  jijini Dodoma , Wakati akitoa taarifa ya utekelezaji  wa miradi ya maendeleo  ya robo tatu ya mwaka katika kikao cha Baraza la Madiwani kilicho fanyika Jijini hapa.

Aidha, kunambi ameongeza kuwa  changamoto ya sekta ya ardhi ni changamoto ya kihistoria kwani iliyokuwa Manispaa haikuwa na fursa ya kupanga  wala kufanya maamuzi kwenye sekta ya ardhi na kwa muda mrefu takribani miaka  43 iliyokuwa mamlaka ya ustawishaji makao makuu ilikuwa ikishughulika  na masuala ya ardhi

''yapo maeneo ambayo kimsingi  ilionekana kama ni changamoto wakati huo ,kwa mfano mwenyekiti iliyokuwa mamlaka ya ustawishaji mwaka 1987 ilipewa hati ya miaka 99 ya jiji la dodoma ilikuwa ndio mamlaka  yenye kupanga kwenye sekta ya ardhi na kutoa viwanja'' alisema kunambi'' Alisema kunambi  

Pia , kunambi amesema Halmashauri ya jiji la Dodoma limechukua  jukumu la kuweza kutatua kero hizo

Naye Diwani wa kata ya Chang’ombe  Bakari Fundikili ameipongeza  ofisi ya Mkurugenzi ,ofisi ya mkuu wa Wilaya na ofisi ya Mkuu wa mkoa hatua walio ichukua kwaajili ya kutatua migogoro hiyo.


Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antoy Peter Mavunde ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, Sera, Bunge,kazi,ajira na vijana   amesema kuwa amefurahishwa na utaribu uliowekwa kupitia ofisi ya mkurugenzi na mkuu wa wilaya kwaajili ya kutembelea maeneo yote yenye kero kwaajili ya kusikiliza wananchi .


Hatahivyo, Mavunde amesema kuwa watendaji chini ya ofisi ya mkurugenzi wamekuwa wakifanya vizuri katika sekta ya ardhi kwani hivi sasa malalamiko hayo yamepungua.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.