Header Ads

Wizara ya kilimo yajipanga kukabiliana na uhaba wa chakula


Wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha inakabiliana na uhaba wa chakula kutokana na tishio la ukame kwa kutenga jumla ya Sh. Bilioni 24 za kununulia chakula na kuhifadhi.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba ametoa kauli hiyo bungeni,  jana Jumatano, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Babati Mjini, Paulina Gekul (CCM) aliyetaka kujua serikali imejipanga vipi kukabiliana na tishio la uhaba wa chakula kutokana na maeneo ya kaskazini kukosa mvua.

Mgumba alisema kutokana na tishio hilo litokanano na mabadiliko ya tabia nchi, wizara imejipanga kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Tanzania (NFRA) kwa kutenga Sh bilioni 15 kununulia mahindi na kuhifadhi.

Alisema wizara imewatuma watalaamu kutoka katika wizara hiyo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuona ukubwa wa athari ya ukame na uhaba wa mvua na chakula ili kujua ukubwa wake,"alisema

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.