Header Ads

WWF latoa wito huu kwa wadau wa maendeleo
Shirika la uhifadhi wa mazingira Duniani (WWF) limetoa wito kwa wadau wa maendeleo nchini kuacha kutegemea matukio maalumu katika zoezi la  upandaji misitu.

Wito huo umetolewa leo katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko na Ofisa Program ya Misitu wa WWF, Azaria Kilimba. Wakati wa hafla ya uzinduzi wa upandaji miti katika mkoa wa Lindi.

Kilimba alisema zoezi la upandaji miti linatakiwa kuwa endelevu, badala ya kutegemea matukio maalumu. Ikiwemo ya kitaifa na kimataifa yanayohusu utunzaji mazingira na upandaji miti.

Ofisa huyo wa WWF alisema iwapo wadau wa maendeleo wanaunga mkono jitihada za serikali katika kuinusuru nchi isigeuke jangwa, hawanabudi kulifanya zoezi la upandaji miti kuwa endelevu. Badala ya kusubiri matukio maalumu.

"Kama tunaunga mkono azima ya serikali ya kuwa nchi ya viwanda,  nilazima upandaji miti uwe endelevu. Sisi(WWF) tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na wanyama pori,"  Kilimba alisisitiza na kuhaidi.

Hafla hiyo ya uzinduzi wa upandaji miti kimkoa ilifadhiliwa na WWF, MCDI, Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi,mkuu wa wilaya ya Kilwa na halmashauri ya wilaya ya Killwa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.