Header Ads

yanga kuwakosa wacehzaji hawa


Yanga kesho watakuwa ugenini kucheza mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, kuelekea mchezo huo Yanga itawakosa Kelvin Yondani na Feitoto lakini Ibrahim Ajibu na Ninja wanarejea.

Kelvin Yondan alipata kadi nyekundu mechi iliyopita, Feisal Salum 'Feitoto' alipata kadi ya tatu ya njano kwa hiyo wote wataukosa mchezo wa Yanga vs Mtibwa.

Ajibu alikuwa majeruhi amerudi na kocha amesema anaweza kumpa nafasi ya kucheza kidogo ili kujiweka sawa kwa ajili ya mechi dhidi ya Azam. Abdallah Shaibu 'Ninja' anarejea baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi nne.

Kocha wa Yanga Zahera Mwinyi anasema: "Hakuna tofauti wawili wanatoka, wawili wanaingia."

"Tuliweka malengo kwamba, kabla ya kucheza na Azam tunatakiwa kushinda mechi zetu zote. Tumeshashinda mbili imebaki dhidi ya Mtibwa lakini tukifanya kama tulivyofanya Mwanza itakuwa vizuri."

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.