Header Ads

Yanga mbioni kumsajili mshambuliaji hatari


Taarifa inaeleza kuwa Klabu ya Yanga ipo katika harakati za kumsajili mshambuliaji hatari wa klabu ya FC Lupopo ya DR Congo, Roderick Mutuma.

Klabu ya Yanga tayari imetuma maombi ya kumsajili nyota huyo raia wa Zimbabwe mwenye thamani ya dola 113,000 ambazo ni zaidi ya milioni 260 za Kitanzania.

Jeuri ya Yanga kufanya usajili huo inakuja kutokana na harambee ya kuichangia klabu iliyozinduliwa hivi karibuni Dodoma kwa ajili ya kuchanga fedha.

Kocha wa Yanga SC, Mwinyi Zahera tayari ameshaanza kujinadi kuwa usajili wa msimu ujao utakuwa ni waina yake ili kukiboresha kikosi.

Zahera aliahidi kuwa kwa fedha ambazo zitachangishwa na wanachama pamoja na mashabiki wa timu hiyo zitasaidia katika kununua wachezaji wa maana ndani ya timu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.